01.
Unda na ujaze tena Pochi yako ya Mwekezaji
Jisajili kwenye JustMarkets na ujaze tena Pochi yako ya Mwekezaji kupitia njia yoyote ya malipo unayoipenda. Unaweza kuhamisha fedha kwenda kwenye Pochi yako ya Mwekezaji kwa kutumia uhamishaji wa ndani ikiwa tayari una pesa kwenye moja ya akaunti zako za JustMarkets.
02.
Fuatilia wafanyabiashara bora
Tafuta Wafanyabiashara unavyotaka kuwekeza kwao, kisha ubofye ‘Anza kunakili.’ Biashara zao zitanakiliwa kiotomatiki. Diversify portfolio yako kwa mikakati mbalimbali.
03.
Fuatilia na upate faida
Nenda kwenye Eneo la Mwekezaji na uangalie kiashiria chako cha faida, hariri, au usimamishe mchakato wa kunakili wakati wowote. Nakili Wafanyabiashara wengi kadiri unavyotaka na upokee mapato yanayotegemeka.
JustMarkets Copytrading hukuruhusu kunakili wafanyabiashara wengine na kufaidika kutokana na mafanikio yao.
Faida za kujiunga na JustMarkets Copytrading
MASWALI YANAYOULIZWA MARA NYINGI
1
Ninachaguaje Mfanyabiashara?
Ukadiriaji wa Mfanyabiashara katika Ubao wa Viongozi unategemea kiashiria cha faida kinachoonyesha jinsi mkakati wa Mfanyabiashara ulivyofanikiwa. Kwa kutumia kiashiria hiki, unaweza kuchagua kuwekeza na Mfanyabiashara aliyefanikiwa zaidi.
2
Jinsi ya kuchagua Wafanyabiashara wa kuwanakili:
Takwimu za Mfanyabiashara zinajumuisha utendaji na idadi ya Wawekezaji, tozo, jozi za biashara ambazo Mfanyabiashara hutumia, kipengele cha faida, mwelekeo wa oda, na vipengele vingine vingi ambavyo unaweza kuvikagua kabla ya kufanya uamuzi wako wa kumnakili mtu. Kabla ya kuanza, unapanga asilimia ya fedha utakazoweka na kuchagua kiasi cha kuwekeza na Mfanyabiashara mahususi.
3
Chaguo la Hali ya Kunakili kwa Wawekezaji ni nini?
Kuchagua «Hali ya Kunakili» kunamruhusu Mwekezaji kuanza kunakili biashara kwa kubainisha uwiano wa maagizo ya kunakili, yaani, Inayolingana (x1), Maradufu (×2), Mara Tatu (×3), au kiasi kingine chochote Maalum, kuelekea juu na chini. Iwapo kiasi cha biashara inayonakiliwa na Mwekezaji kinakuwa chini ya kiwango cha chini kinachohitajika cha fungu 0.01 – biashara itafunguliwa kwa kiwango cha chini kinachohitajika.
Mfano wa 1: Mwekezaji ameweka kizidishaji Maradufu (×2) na fungu moja la biashara limefunguliwa kwenye Akaunti ya Mfanyabiashara. Kiasi cha biashara iliyoigwa kitakuwa: fungu 1 x kizidishaji 2 = mafungu
2.
Mfano wa 2: Mwekezaji ameweka kizidishaji Maalum (×0.5) na fungu moja la biashara limefunguliwa kwenye Akaunti ya Mfanyabiashara. Kiasi cha biashara iliyonayoigwa kitakuwa: fungu 1 x kizidishaji 0.5 = fungu 0.5.
4
Je, mnatoza tozo yoyote kwa kunakili Wafanyabiashara?
JustMarkets haitozi tozo yoyote ya ziada, lakini unalipa tozo ya Mfanyabiashara, ambayo imebainishwa kibinafsi kama asilimia ya faida yako. Tozo inatozwa kwa Dola za Marekani.
5
Je, ninaweza kuacha kumnakili Mfanyabiashara?
Unaweza kujiondoa na uache kumnakili Mfanyabiashara na biashara zake wakati wowote. Unapojiondoa, fedha zote zilizowekezwa katika Mfanyabiashara na faida yoyote iliyotokana na kumnakili Mfanyabiashara huyu hurejeshwa kwenye Pochi yako ya Mwekezaji.
Kabla ya kujiondoa, tafadhali hakikisha biashara zote za sasa zimefungwa.