Kalenda ya mambo ya kiuchumi
Economic Calendar by Myfxbook.com
Kalenda ya Mambo ya Kiuchumi Ni Nini
Kalenda ya mambo ya kiuchumi ni nyenzo inayoorodhesha matukio yote muhimu ya kiuchumi. Baadhi ya kalenda pia hutia ndani viashiria muhimu, fahirisi na ukadiriaji.
Kalenda ya mambo ya kiuchumi ya JustMarkets inatoa:
- Matukio zaidi ya 1000 ya mambo ya kiuchumi;
- Ufuatiliaji wa moja kwa moja kulingana na wakati halisi kwa nchi zaidi ya 50;
- Uainishaji kulingana na athari ya tukio;
- Saa za maeneo husika zinazoweza kubadilishwa kulingana na eneo lako;
- Programu za Android na iOS.
Tunasasisha kalenda mara kwa mara kwa msaada wa mamilioni ya waandishi wa habari kutoka ulimwenguni kote. Data zinakuja mubashara saa 24 kwa siku, siku 5 kwa wiki. Chochote kitakachotokea, sikuzote tunahakikisha kuwa una habari za hivi karibuni zaidi na data zinazokufaa zaidi.
Matukio ya Kiuchumi Ni Nini
Matukio ya kiuchumi ni taarifa za habari, machapisho ya ripoti, taarifa za maafisa wa serikali na vyombo vingine vya habari ambazo zinaweza kuathiri bei ya dondoo za Fedha za Kigeni.
Hapa kuna mifano ya matukio muhimu ya kiuchumi:
- Machapisho ya Ripoti ya GDP;
- Chapisho la Kumbukumbu za FOMC;
- Sasisho la Utafiti wa Nafasi za Kazi na Mzunguko wa Ajira;
- Hotuba ya Rais wa ECB Kuhusu Kiwango Kikuu cha Riba;
- Kura ya Bunge la Uingereza Kuhusu Uingereza Kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya.
Siyo matukio haya yote yana nguvu sawa, lakini kila moja lina umuhimu wa kiuchumi na hakika litaathiri soko na kusababisha ama kununua kwa wingi au kuuza kwa wingi.
Kwa Nini Wafanyabiashara Wanahitaji Kalenda ya Kiuchumi
Uchumi ni taaluma inayohusiana sana na matukio ya ulimwengu halisi. Na biashara ya Forex, ambayo hutumia kanuni za kiuchumi kwa vitendo, ni uthibitisho wa hilo. Hivyo basi, ingawa mifumo ya kihisabati na mbinu nyingine kama Hatua ya Bei huwa ya kutegemewa mara nyingi, huwa haina maana sana wakati tukio kubwa linapotokea katika ulimwengu halisi.
Kalenda za kiuchumi hutoa data kwa ajili ya uchambuzi wa kina na kusaidia kutabiri mwelekeo ambao soko la Forex litachukua siku za usoni. Kwa kawaida, hutumiwa zaidi na wale wanaofuata uchambuzi wa kimsingi. Baadhi ya mikakati ya biashara ya Forex, kama vile biashara ya haraka kwa faida ndogo, imejengwa kwa kutumia kalenda za kiuchumi kutabiri mabadiliko makubwa sokoni na kufanya biashara ili kunufaika nayo.
Hata hivyo, hata iwapo huamini sana uchambuzi wa kimsingi wa kiuchumi na unafuata mikakati ya Hatua ya Bei, bado unaweza kutumia Kalenda ya Kiuchumi ili kuona ni lini soko linaweza kuathiriwa na matukio ya ulimwengu halisi.
Jinsi ya Kutumia Kalenda ya Kiuchumi
Kalenda ya kiuchumi ya JustMarkets inaorodhesha matukio yote yanayohusiana na biashara kwa mpangilio wa wakati.
- Safu ya kwanza inaonyesha tarehe na saa kamili ambapo tukio litatokea;
- Safu ya pili inaonyesha muda uliosalia hadi tukio lianze;
- Safu ya tatu ina jina la tukio, pamoja na bendera ya nchi ambako tukio hilo litafanyika;
- Safu ya nne inaeleza kiwango cha athari ambacho tukio hilo litakuwa nacho kwenye soko na kiwango cha mtetemo kinachoweza kusababishwa;
- Safu ya tano inaonyesha mabadiliko yanayotarajiwa ambayo tukio hilo litasababisha kwenye thamani ya sarafu husika;
- Safu ya sita hurekebisha utabiri wa awali ikiwa kuna haja ya kufanya hivyo;
- Safu ya saba hujazwa tu baada ya tukio kumalizika na inaonyesha athari halisi ambayo tukio hilo lilikuwa nayo kwenye sarafu.
Unaweza pia kubofya kila tukio ili kuona maelezo yake, pamoja na kiungo cha kusoma taarifa zaidi kuhusu tukio hilo.
KUMBUKA: Ikiwa unafanya biashara ya sarafu kuu pekee na hutaki kufanya uchambuzi wako mwenyewe – angalia sehemu yetu ya Muhtasari wa Soko na Utabiri wa Kila Siku. Huko utaona matukio muhimu zaidi, pamoja na maelezo ya jinsi hasa yatakavyoathiri soko.
Jinsi ya Kuchuja Matukio Yasiyo Muhimu
Kama unahisi kuna matukio mengi yasiyo na umuhimu kwako – usijali, unaweza kuyachuja yale usiyoyahitaji. Ili kufanya hivyo, bofya kitufe cha “Zaidi” kisha weka mipangilio ya kichujio kulingana na mahitaji yako.
Hapa unaweza kuondoa sarafu ambazo kwa sasa hufanyi nazo biashara, pamoja na matukio ya athari ndogo ambayo hayawezi kusababisha mtetemo wa soko wa kutosha kuzingatia.

