Nunua na Kuuza Fahirisi za Hisa ukiwa na Hali Bora za Biashara

Tawala soko la fahirisi za hisa na JustMarkets ukiwa na hali za biashara zinazoendana na mbinu yako ya kimkakati.

hero indices

Kwa nini ufanye biashara ya fahirisi za hisa ukiwa na JustMarkets?

Kuanzia fahirisi za hisa za NASDAQ inayoendeshwa kwa teknolojia hadi fahirisi pana zaidi ya S&P, JustMarkets inakupa makali katika soko la fahirisi za hisa za kimataifa zenye ushindani mkubwa, na kuhakikisha umejiandaa kwa ajili ya mafanikio.

benefits-1

Aina tofauti tofauti za fahirisi za hisa

Ukiwa na JustMarkets, unaweza kuchunguza fahirisi mbalimbali za hisa kutoka duniani kote kama vile Dow Jones, NASDAQ, FTSE100 au NIKKEI ili kupanua uwekezaji wako katika biashara.

benefits-3

Tofauti Ndogo & Isiyobadilika Badilika kati ya bei ya kununua na kuuza

Fanya biashara ya fahirisi za hisa za Dow Jones, S&P 500, au NASDAQ zenye tofauti ndogo mno kati ya bei ya kununua na kuuza ikianzia pips 0.0, kuhakikisha utulivu hata wakati ambapo soko linabadilikabadilika mno.

benefits-6

Utekelezaji wa oda haraka

Katika JustMarkets, dili zako zinafanywa papo hapo. Ndani ya sekunde tu, tunahakikisha kuwa biashara zako zinatekelezwa, na kukupa kasi unayohitaji ili kufanya biashara kwa ufanisi.

benefits-4

Kutoa fedha papo hapo

Pata pesa zako haraka unapotaka kuzitoa. Chagua kutoka kwenye njia mbalimbali za malipo na upate idhini ya haraka kwa maombi yako.

benefits-2

Biashara ya kubadilisha bila riba

Kila mfanyabiashara katika JustMarkets anaweza kufanya biashara bila riba ya ubadilishaji na hakuna matakwa ya ziada, akiruhusiwa kufanya biashara bila malipo ya ziada.

benefits-5

Ulinzi dhidi ya mabadiliko ya bei yenye athari hasi

Fanya biashara bila wasiwasi ukiwa na ulinzi wetu dhidi ya mabadiliko ya bei yenye athari hasi. Inazuia mabadiliko ya bei yenye athari hasi, kwa hivyo biashara zako huanzia na kuishia pale unapotarajia, bila kukosa mabadiliko yoyote madogo ya bei.

Tofauti kati ya bei za kununua na kuuza na riba za ubadilishaji kwenye soko la fahirisi za hisa

Tofauti ya bei wastani

 

pips

Kamisheni

 

kwa kila loti/ndani

Dhamana

 

hadi 1:500

Malipo ya usiku mrefu

 

Pointi

Malipo ya usiku mfupi

 

Pointi

Kiwango cha kuzuia*

 

pips

Hali za soko la fahirisi za hisa

Ukiwa na JustMarkets, unaweza kuingia kwenye mtandao mkubwa wa soko la kimataifa, lenye idadi kubwa ya fahirisi za hisa – kuanzia zile za makongamano ya kimataifa hadi kampuni zinazobadilikabadilika zenye mtaji mdogo. Tovuti yetu hukuruhusu kufuatilia mienendo ya soko na kujipatia faida kutokana na mabadiliko ya bei katika fahirisi zote za hisa.

Saa za kufanya biashara

Zana Kufungua Kufunga
AU200, DE40, EU50, FR40, HK50, JP225, UK100, US100, US30, US500, CHA50 Jumatatu 01:02
Mapumziko ya kila siku 23:59 – 01:02
Ijumaa 23:59
ES35 Jumatatu 09:02
Mapumziko ya kila siku 20:59 – 09:02
Ijumaa 20:59

Muda wote uko katika wakati wa seva (GMT+2).

Tofauti kati ya bei za kununua na kuuza

Tofauti kati ya bei ya kununua na kuuza katika soko la fahirisi za hisa mara nyingi hubadilikabadilika. Tofauti kati ya bei za kununua na kuuza zilizotajwa hapo juu ni wastani uliopatikana kutoka katika biashara za siku za awali. Angalia tovuti yetu ili kuona tofauti kati ya bei ya kununua na kuuza kwa sasa.

Tofauti kati ya bei za kununua na kuuza zinaweza kuongezeka wakati wa ukwasi mdogo au mabadiliko makubwa katika soko. Hii inajumuisha nyakati kama vile wakati wa mgeuko wa soko, habari mpya kuhusu soko, na matoleo mapya na inaweza kuendelea hadi hali ya kawaida katika soko itakapoanza tena.

Tofauti zetu bora kati ya bei ya kununua na kuuza ni hakika kwenye akaunti yetu ya Raw Spread, ambapo tofauti kati ya bei ya kununua na kuuza huanzia pips 0.0.

Biashara ya kubadilisha bila riba

Riba ya ubadilishaji ni ada inayotozwa kwenye nafasi za biashara za fedha za kigeni ambazo zinabaki wazi usiku kucha. Riba ya ubadilishaji hutofautiana katika jozi tofauti za sarafu. Riba za ubadilishaji hutozwa saa 4:00 usiku GMT+2 kila siku, bila kujumuisha wikendi, hadi nafasi itakapokuwa imefungwa. Ni muhimu kutambua kwamba kwa biashara yenye jozi za fedha za kigeni, riba za ubadilishaji kwa siku ya Jumatano huongezeka mara tatu ili kugharimia gharama za riba za wikendi.

Hutatozwa kwa fahirisi za hisa zilizowekewa alama ya “Waliokubaliwa Ubadilishaji bila riba wanaruhusiwa” katika jedwali hapo juu ikiwa una hali ya ubadilishaji bila riba.

Akaunti zote za wateja kutoka nchi yoyote hupewa moja kwa moja hali ya ubadilishaji bila riba.

Kiwango cha kusitisha

Kiwango cha amri ya kusimamisha biashara ndio umbali wa chini zaidi unaokubalika kati ya bei unayotaka kufungua nafasi nayo na bei ya sasa ya soko wakati unapoweka oda inayosubiri (kama vile Zuia Hasara, Chukua Faida, Kuuza kwa amri ya kusubiri bei ipande/ Kuuza kwa amri ya kusubiri bei ishuke, au Kipimo cha kunua kwa bei ya chini/ Kipimo cha kuuza kwa bei ya juu). Kiwango hiki husaidia kupunguza hatari ya mabadiliko ya ghafla ya bei (mtelezo wa bei) wakati wa kipindi cha mabadiliko makubwa ya soko, na huhakikisha utekelezaji wa uhakika zaidi wa oda zinazosubiri.

Zingatia kwamba kiasi katika kiwango cha kusitisha kilichoonyeshwa kwenye jedwali hapo juu kinaweza kubadilika na huenda kisiweze kutumiwa na wafanyabiashara wanaotumia mikakati mahususi ya kuchakata oda nyingi haraka au kutumia Washauri Wataalamu.

Matakwa ya kiasi cha dhamana kisichobadilika

Kwa biashara ya fahirisi za hisa, kiwango cha kujiinua kisichobadilika ni 1:500 kwa US30, US500, na US100, wakati kwa fahirisi zingine zote za hisa, kinabaki kuwa 1:200.

Matakwa ya kiasi cha dhamana kwa ajili ya fahirisi zote za hisa yanabadilika kulingana na fahirisi hususa. Orodha ya kina ya matakwa yaliyoboreshwa ya kiasi cha dhamana kwa ajili ya fahirisi za hisa yanapatikana hapa.

Programu ya simu ya JustMarkets

Tambua fursa, fanya biashara na udhibiti akaunti zako za biashara ukitumia programu ya JustMarkets Trade. Furahia urahisi wa kuwekana kutoa pesa, machaguo mengi ya njia za malipo na usaidizi wa ndani ya programu kwa saa 24 siku 7 za juma.

Tumia skana kupakua programu

iOS na Android

Phone in a hand

Maswali yanayoulizwa mara nyingi

1
Kwa nini zinaitwa fahirisi za hisa?

Katika mambo ya fedha, maneno fahirisi za hisa hurejelea kipimo cha takwimu au kiashiria kinachowakilisha utendaji wa sekta maalum au sehemu ya soko la hisa. Fahirisi huitwa hivyo kwa sababu zinaonyesha au kupima mienendo ya bei ya pamoja ya kundi fulani la hisa.

2
Mifano ya fahirisi za hisa ni ipi?

Mifano ya fahirisi maarufu za hisa inatia ndani Dow Jones Industrial Average (DJIA), Standard & Poor’s 500 (S&P 500), na Nasdaq Composite nchini Marekani. Kimataifa, kuna fahirisi za hisa kama FTSE 100 nchini Uingereza, DAX nchini Ujerumani, na Nikkei 225 nchini Japani.

3
Ni fahirisi gani 3 ambazo ni kubwa zaidi?

Fahirisi tatu kubwa, inapohusu umaarufu wazo katika kutambuliwa na kutumiwa kama viashiria vya kiuchumi, ni S&P 500, ambayo inaonyesha utendaji wa makampuni makubwa 500 yaliyoorodheshwa kwenye masoko ya hisa ya Marekani; Dow Jones Industrial Average (DJIA), inayowakilisha makampuni makubwa 30 yanayomilikiwa na umma; na Nasdaq Composite, inayojulikana kwa kujumuisha idadi kubwa ya hisa za teknolojia.

4
Je, kuna faida gani za kufanya biashara kupitia mabadiliko ya bei za fahirisi za hisa badala ya kuwekeza katika fahirisi za hisa?

Kufanya biashara kupitia nyenzo zinazopima mabadiliko ya bei za fahirisi ya hisa, kama vile mikataba ya baadaye na haki ya kununua hisa, hutoa fursa zenye faida kama vile uwezo wa kujiinua, ambao unakuruhusu kufanya biashara kubwa ukiwa na mtaji mdogo. Pia hukupa uwezo wa kufanya mabadiliko unapotekeleza mikakati mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mkakati wa kujilinda. Biashara ya nyenzo zinazopima mabadiliko ya bei za fahirisi ya hisa inaweza kufanywa kupitia dhamana na inatoa fursa ya kufaidika kutokana na masoko yanayokua na yale yanayoanguka, tofauti na uwekezaji wa moja kwa moja katika fahirisi za hisa.

5
Ni wakati gani mzuri wa kufanya biashara ya fahirisi za hisa?

Wakati mzuri wa kununua au kuuza fahirisi za hisa kwa ujumla unaendana na saa za kufanya biashara za hisa husika. Kwa fahirisi kuu kama vile S&P 500 au DJIA, biashara inakuwa kileleni wakati wa saa za kawaida za kufanya biashara za soko la hisa la Marekani, hasa saa za kwanza na za mwisho za siku ya biashara wakati kiasi cha biashara na mabadiliko ni makubwa.

6
Ni viashiria gani ninavyoweza kutumia kwenye chati ya fahirisi ya hisa?

Kwenye chati ya fahirisi ya hisa, viashiria maarufu vya kiufundi ni pamoja na wastani unaosogea kwa ajili ya kutambua mwenendo, Relative Strength Index (RSI) kwa ajili ya kutathmini hali za kununuliwa kupita kiasi au kuuzwa kupita kiasi, Bollinger Bands kwa ajili ya uchambuzi wa mabadiliko ya bei, na Moving Average Convergence Divergence (MACD) kwa ajili ya kutambua ishara za uwezekano wa kununuliwa na kuuzwa.